WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

WELCOME "KARIBU" TO ORANGE FOOTBALL ACADEMY ZANZIBAR

.

.

.

.

.

.

MUDATHIR YAHYA

MUDATHIR YAHYA

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

SEIF ABDALLA "karihe"

SEIF ABDALLA "karihe"

.

.

.

.

.

.

.

.

.

.

www.ofaznz.net

Total Pageviews

Tuesday 2 January 2018

Chipukizi wanao tandaza soka ya kitabuni

Vijana wa Zanzibar city wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya pambano lao na zantel ambapo waliweza kuwachapa jumla ya mabao 2-1 katika pambano kali na ufundi wa hali ya juu lililotawaliwa na kila aina ya ufundi kutoka katika idara zote za Zanzibar city iliyo Sheheni  vipaji ambavyo ni msaada mkubwa kwa Taifa hapo baadae.

Monday 26 December 2016

JE UNAJUA KWAMBA TANZANIA INA TIMU 4 CAF ?

Mara nyingi kumekuwa na mtazamo kuwa Tanzania inawakilishwa na timu 2 katika mashindano ya Orange Champions League na kombe la washindi wa pili huku  ukweli ni kuwa Tanzania inawakilishwa na Timu 4, mbili kombe la Mabingwa na 2 kombe la Washindi wa pili .

Kutokana na mambo ya kutojielewa Tanzania imekuwa ikipoteza nafasi zao hizo 4 na kujikuta ikibakiwa na nafasi ambazo zinawakilishwa na timu za Tanzania Bara huku ikisahau zile nafasi mbili za Zanzibar kuwa ni nafasi nyingine mbili za ziada za Tanzania.
Kutokana na ratiba za michuano hio nadhani unaweza kugundua kwamba timu za Tanzania Bara hupata wakati mgumu sana katika ratiba zao kwa kuangukia mara nyingi katika timu za nchi za Afrika kaskazini huku timu za upande wa Zanzibar zikianza mara nyingi na nchi tofauti za kusini mwa Afrika, kutokana na udhaifu au mfumo mbovu wa mashindano ya ligi ya Zanzibar inazifanya timu zake kuyaaga mara moja tu baada ya kucheza mechi zao za awali za nyumbani na ugenini hivyo Tanzania katika hali ya kutojitambua imekuwa ikipoteza timu mbili kila mwaka za Zanzibar katika hatua za mechi zao za kwanza kabisa hivyo kubakiwa na timu mbili za Bara ambazo kwa bahati mbaya nazo mara huangukia mikononi mwa Waarabu na kuanza tena stori hio miaka yote.
Kutokana na kutojitambua huko Tanzania inabakia kuwakilishwa kiakili na timu 2 yaani mbili kutoka Tanzania Bara, na pia timu mbili Tanzania Visiwani hapo nikimaanisha hakuna Muungano katika soka la umoja ambao unahusisha mikakati ya kuziboresha timu za pande mbili na kukomaa katika mshindano yaho makubwa barani Afrika kwa vilabu hivyo kubaki kila upande na timu mbili kivyake.

Muda umefika kwa viongozi wa pande mbili Bara na Visiwani kuanza mikakati mipya ili timu 4 ambazo ni nafasi nyingi kwa Tanzania kuweza kuzifanyia usahihi na kuwa na wawakilishi bora barani Afrika.
Kama nchi za Zambia zina wawakilishi 2 na kufika mbali katika mashindano ya Afrika ni wakati wa Tanzania yenye timu 4 kufika mbali zaidi kuliko timu hizo mfano waa  kama Zambia.
Tunaomba viongozi wahusika wa pande zote mbili kukaa pamoja na KU-fix matatizo madogo madogo ili kuinua kiwango cha Soka nchini, Soka ni Ajira kubwa duniani kote hivyo Viongozi wahusika wasiendelee kuzorotesha Ajira za vijana na watu wengi nchini, huu ni muda muwafaka na kuanza teza hii kazi iliyozorota kwa miaka mingi.

Sunday 27 November 2016

RECORD ZA MABAO

De meest verbluffende records uit de voetbalwereld



 Tarehe 22-9-2015 Mchezaji wa Byern München  Robert Lewandowski alipachika mabao 5 ndani ya dakika 9 tokea akitua uwanjani, huku akitokea kwenye benchi timu yake ya Bayern München ikiwa nyuma kwa bao 1-0 dhidi ya Wolfsburg katika mechi ya Bundasliga iliyofanyika katika uwanja wa Allianz-Arena, Mechi hio ilihudhuriwa na washabiki 75,000 katika uwanja huo wa nyumbani wa Bayern Munchen , mkali huyo wa mabao aliyatwanga mabao hayo katika dakika za R. Lewandowski 51', 52', 55', 57', 60'
Op 22 september 2015 scoorde Bayern Munchen's aanvaller Robert Lewandowski, maar liefst vijf keer in negen minuten tijdens een invalbeurt. De voetballer en zijn club stonden met 1-0 achter toen hij in de tweede helft mocht spelen en hij scoorde meteen vijf keer. Klik verder voor meer verbluffende voetbalrecords.
.............................................................................................................................................

Golkipa namba 1 wa zamani wa timu ya Taifa ya Paraguay Jose Luis Chilavert akiwa ni kipa aliyesifika kwa kupachika mabao ya mipira iliyokufa yaani freekick pamoja na Penalti aliandika record pale alipofunga Hattrick mwaka 1999 wakati timu yake ya Vélez Sarsfield ilipocheza dhidi ya Ferro Carril East
Paraguay’s keeper Jose Luis Chilavert staat bekend om zijn scorend vermogen is de meest scorende keeper ter wereld na de Braziliaan Ceni. Chilavert werd echter wereldnieuws toen hij een hattrick maakte. Hij deed dit voor Vélez Sarsfield tegen Ferro Carril Oeste in 1999.
..................................................................................................................................

Wachezaji Wakalikama Pele, Maradona, Messi, Christiano Ronaldo wana records nyingi za mabao za timu ya Taifa, lakini mchezaji mkali wa zamani wa timu ya Taifa ya Iran na Bayern  München Ali Daei aliipachikia  timu ya Taifa ya Iran julma ya mabao109 ndani ya mechi 149 alizocheza.
Spelers als Diego Maradona, Lionel Messi, Christiano  en Pele hebben allemaal grote records op hun naam staan maar de international die het vaakst gescoord heeft is Iran’s Ali Daei, die 109 maal het doel trof in 149 wedstrijden.
............................................................................................................................

Inaonekana kama Pele wa Brasil ndio mchezaji aliefunga mabao mengi katika historia ya mchezo wa soka, lakini uhakika ni kwamba ni Josef Biscan kutoka Austria-Tsjechoslovakia alietundika mabao 1468 katika mechi 918 alizocheza, huku Pele akiwa ni namba mbili katika kitabu cha Guinness Records, kwasababu hesabu za miaka ya 30' , na  40' imeondolewa katika hesabu kutoka na figisufigisu za hesabu za miaka hio. 


Braziliaanse legende Pele wordt gezien als de speler met de meeste doelpunten in zijn carrière, maar het is eigenlijk Josef Biscan, die uitkwam voor Oostenrijk en TsjechoSlowaijke, die 1468 keer scoorde in 918 wedstrijden. Pele staat echter in het Guinness Book of Records, omdat de tellingen uit de jaren '30 en '40 niet meer als betrouwbaar worden gezien.
........................................................................................................................

Golkipa wa zamani wa Sao Paulo Rogerio Ceni ndio anaongoza kwa mabao huku akiwa ni mlinda mlango, kinara huyo wa mabao ambae hakuwahi kufunga hata mara moja Hattrick alipachika kambani mabao 130 kati ya mechi 600 alizolinda goli.
Sao Paulo keeper Rogerio Ceni heeft met 130 doelpunten in meer dan 600 wedstrijden als keeper het vaakst gescoord.
.................................................................................................................................

Mshambuliaji wa Russia Oleg Salenko ndie mchezaji anayeongoza kupiga mabao katika timu za Taifa katika michuano ya Kombe la Dunia, alifanya hivyo baada ya kupachika kambani mabao 5 wakati wa kombe la dunia Russia dhidi ya Cameroon mwaka 1994.
De Russische Oleg Salenko scoorde vijf keer in Rusland's overwinning tegen Kameroen tijdens het WK van 1994.
...................................................................................................................................................
On 14 March 2013, Torres scored the third goal as Chelsea defeated Steaua București 3–1 to advance 3–2 on aggregate to the quarter-final of the Europa League. With this goal, Torres became the first player to score in seven different competitions in one season.

Other Competitions  Primier League, Champions League, Europer League, FIFA Club World Cup, Fa Community Shield, FA Cup, League Cup.
.....................................................................................................................................

Zlatan Ibrahimovic na Christiano Ronaldo ndio wachezaji pekee wanaoshikilia records za kupachika mabao kwa dakika zote za mchezo wa soka, wamefanya hivyo kila mmoja wao kwa kupachika bao katika dakika ya 1 ya mchezo, dakika ya 2 na kuendeleza hivyo hadi dakika 90 mchezo katika mechi mbalimbali walizocheza kila mmoja wao.
Cristiano Ronaldo en Zlatan Ibrahimovic zijn de enige twee spelers in de geschiedenis die in elke minuut van de wedstrijd hebben gescoord, 1-90. Uiteraard niet in dezelfde wedstrijd.
......................................................................................................................................

Golkipa wa zamani wa Stoke City ndio anayeongoza kwa kupachika bao akiwa umbali wa urefu wa mita 91.
De voormalig keeper van Stoke City goalkeeper Asmir Begovic wist een goal van 91 meter afstand te maken.
.........................................................................................................

Zlatan Ibrahimovic ni mchezaji pekee aliecheza katika vilabu 6 tofauti na kufunga mabao katika michuano ya Champions League kwa kila klabu aliyochezea
Zlatan Ibrahimovic heeft voor zes verschillende clubs gespeeld en gescoord in de UEFA Champions League.
.....................................................................................................................

Katika michuano ya kombe la dunia mwaka 1982 Timu ya Taifa ya Hungary iliichapa El Salvador jumla ya mabao 10 hivyo kuwa record kubwa kutokea katika hatua ya fainali za michuano hio mikubwa duniani katika soka.
Hongarije heeft de meeste doelpunten ooit gescoord in een wedstrijd tijdens het WK toen ze in 1982 van El Salvador wonnen met 10 doelpunten.
.............................................................................................................................................

Super Star kitasa wa Barcelona ametupia kambani mara 5 akiwa na jezi ya timu hio ya Cataluna lakina mabao hayo yote yalikuwa bahati mbaya ni dhidi ya kipa wake yaani mabao ya kujifunga.
Barcelona's Javier Mascherano heeft vijf doelpunten gemaakt voor e Catalanen, maar helaas waren ze allemaal in eigen doel.
...............................................................................................................

Mshambuliaji wa Australia Archie Thompson ndie mchezaji pekee aliyewahi kutokea katika hatua ya awali ya kuwania nafasi ya fainali za kombe la dunia kupachika mabao 13 peke yake katika moja, hio ilikuwa ni Australia dhidi ya Americans Samoa baada ya Australia kuigaragaza Samoa jumla ya mabao 32-0 ndani ya dakika 90.
Australiër Archie Thompson scoorde meeste doelpunten in één international. Amerikaans-Samoa werd met 32-0 verslagen en Thompson scoorde er 13.

Sunday 13 November 2016

UCHANGIAJI WA DAMU ZENJ CHARITABLE SOCIETY

( Katibu mkuu wa kituo cha kukuza soka kwa vijana Orange Football Academy Hussein Ahmada akishiriki katika zoezi la kuchangia damu lililoandaliwa na Zenj Charitable Society sikuya tarehe 11/11/2016 ).


Zenj Charitable Society kwa kushirikiana na Bank ya Damu Zanzibar iliandaa uchangiaji damu wa kujitolea sikuya Ijumaa tarehe 11/11/2016 katika Ofisi ya Zenj Charitable Society Kikwajuni Juu katika Jumba la mkabala na Masjid Sunnah kwa Sheikh Nassour Bachoo,

Uchangia huo wa damu ulikuwa ni kwa lengo la upatikani wa damu kwaajili ya maendeleo ya mtoaji pindipo atahitajia damu siku yoyote pamoja na maendeleo ya Binadamu/ndugu  yako pindipo inapotokea tatizo lolote la msaada wa damu,

Watu walijitokea kuchagia damu ambayo huhifadhiwa katika Bank ya Damu Zanzibar na kusaidiwa wale ambao huhitajia damu hio bila ya kujali ni jamaa au ndugu wadamu wa wachangiaji wa damu,

Mmoja kati ya wachangiaji wa damu siku hio alikuwa ni katibu mkuu wa kituo cha kukuza soka kwa vijana nchini Hussein Ahmada ambae amekuwa akijitokeza na michango na shughuli mbalimbali za maendeleo ya kijamii nchini.

Kwa niaba ya kituo chetu cha kukuza soka kwa vijana nchini tunawashukuru wale wote ambao walijitokeza katika zoezi hilo na kuwaomba wale ambao hawakupata nafasi ya kufika katika zoezi hilo kutokana na michakato na pirika pirika mbalimabli walizokuwa nazo siku kujitokeza kwa wingi mara njingine itakapotokea zoezi kama hilo kwani umuhimu wake sio tu kwa lengo la kuwachangia wanahitajia damu bali hata kwa mtoaji ambapo huwezi kujua ni lini na wapi inaweza kukutokea na ukahitajia msaada wa damu.

WATANO ZANZIBAR WAFAULU MCHUJO U-17 YA AZAM YOUTH ACADEMY

( Mmoja wa nyota wa baadae akimsikiliza mkufunzi wa Azam FC kwa umakini wa hali ya juu ili kumuwezesha kufamu kwa ufasaha na kufanya kile ambacho mwalimu anahitajia kutoka kwake,
hii ni moja kati ya picha kali sana kwa vijana wa umri wake kuwahi kuonekana hapa nchini, ni ya kiwango cha kimataifa na ni mfano kwa vijana wengine nchini kufata mfano huu wa kuigwa, kumsikiliza mwalimu na kufahamu kila kitu ambacho kinarahisisha katika utendaji wake ndani na nje ya uwanja pamoja na ndio hupelekea mchezaji kufikia malengo kutokana na mpango huu mchezaji anaojijengea tokea akiwa na umri mdogo ).




Makinda watano Zanzibar wamechaguliwa kujiunga na timu ya vijana chini ya umri miaka 17 ya Azam FC baafa ya usajili uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita visiwani humo.

Vijana hao wameingia kwenye mchujo wa mwisho utakaofanyika mwezi ujao makao makuu ya Azam, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam yakihusisha vijana wote waliochaguliwa kwenye mikoa mbalimbali.

Vijana hao watano wanaungana na wengine 37 waliochaguliwa kwenye maeneo tofauti nchini katika mikoa ya Morogoro (12), Dar es Salaam (13), Tanga (12) na kufikisha idadi ya vijana 42 waliochaguliwa mpaka sasa kati ya vipaji 2,143 waliofanyiwa usaili.

Uongozi wa Azam FC kwa kushirikiana na idara ya ufundi ya timu hiyo, umedhamiria kuboresha mfumo wa kituo chake cha kukuza vipaji 'Azam FC Academy' ili kihusishe vijana wa umri tofauti kwa ajili ya kuvuna vipaji vingi zaidi kwa manufaa ya baadaye ya timu hiyo na Taifa kwa ujumla.

Hadi sasa Azam FC imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye uleaji wa vipaji katika kituo hicho, ikivuna vijana kadhaa wanaotamba sehemu tofauti katika timu mbalimbali nchini, wengine wakiwa wanaing'arisha timu kubwa ya kituo hicho.

Baadhi ya waliopandishwa kwenye timu kubwa ni makipa Aishi Manula, Metacha Mnata, mabeki Ismail Gambo, Gadiel Michael, Abdallah Kheri (mkopo Ndanda), viungo Mudathir Yahya, Masoud Abdallah, Bryson Raphael (mkopo Ndanda).

Wengine ni Joseph Kimwaga (mkopo Mwadui), Farid Mussa (aliye mbioni kujiunga na CD Tenerife - Hispania), wshambuliaji Kelvin Friday (mkopo Mtibwa Sugar) na Shaaban Idd.

Wanaotamba na timu nyingine baadhi yao ni Simon Msuva (Yanga), Mohamed Hussein (Simba), Rashid Mandawa (Mtibwa Sugar), Joseph Mahundi (Mbeya City), Jamal Mnyate (Simba).

Wakati huo huo: Azam FC, inatarajia kuendelea kusaka wachezaji chini ya umri wa miaka 17 Jumamosi ijayo Novemba 12 mwaka huu kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 9.00 alasiri ndani ya Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Baada ya wikiendi iliyopita kufanya majaribio ya wazi visiwani Zanzibar, ambako walichaguliwa wachezaji watano, sasa tunarudisha mkazo wetu Tanzania Bara na kufanya majaribio ya mwisho katika jiji la Dar es Salaam.

Kwa majaribio mengine ya wazi katika maeneo mengine kuzunguka Tanzania yatatangazwa hivi karibuni.

SABA WAPITA MCHUJO AZAM ACADEMY DAR





VIJANA saba wenye umri chini ya miaka 17, wamepenya kwenye majaribio ya wazi ya mwisho katika mkoa wa Dar es Salaam, yaliyoendeshwa na Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC leo Jumamosi.
Huo ni mwendelezo wa mpango wa mabingwa hao wa kutengeneza timu bora ya vijana wa umri huo kwa ajili ya kuwatumia kwa miaka ijayo na wengine kunufaika nao kwa kuwauza.
Katika majaribio hayo walijitokeza vijana 433 wenye umri tofauti kuanzia chini ya umri wa miaka 10, 12, 14 na 17, ambapo waliweza kuchaguliwa saba pekee na wengine 33 kuorodheshwa.
Mkuu wa Maendeleo ya Soka ya Vijana Azam FC, Tom Legg, (kulia) akizungumza na kijana aliyejotokeza kwenye majaribio

Mpaka sasa mpango huo umeshahusisha mikoa maeneo matano tofauti nchini katika mkoa wa Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Dodoma na Visiwani Zanzibar, ambako kote kumefanya idadi ya vijana waliofanyiwa usaili kufikia 2,593, kati ya hao 50 pekee ndio waliochaguliwa kushiriki fainali ya mwisho itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex mwezi ujao.

Mbali na hao 50, wengine 96 wameorodheshwa na kuhifadhiwa kama akiba ya baadaye. 

Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana Azam FC, Tom Legg, alisema kuwa amefurashishwa na vijana waliojitokeza kwenye majaribio hayo huku akidai kuwa viwango vilikuwa ni vya hali ya juu.

“Wamejitokeza vijana wadogo sana wanaotoka maeneo ya Chamazi na Mbagala, nimefurahishwa sana kuwaona viwango vilikuwa juu na kiukweli ilikuwa nji nzuri ya kumaliza majaribio Dar es Salaam,” alisema.

Alisema kuwa mara baada ya kumaliza vema zoezi hilo Dar es Salaam, hivi sasa mipango iliyopo ni kuthibitisha tarehe za majaribio mengine ya wazi kwenye maeneo yaliyobakia Tanzania.

Alisema “Kwa sasa tunachoangalia ni kwenda kwenye maeneo mengine manne kwenye mikoa ya Mbeya, Kigoma, Mwanza na tutahudhuria michuanio ya vijana Arusha Desemba mwaka huu, baada ya hapo katikati ya mwezi Desemba tutafanya fainali ya mwisho hapa Chamazi, ambayo itatoa majibu ya timu yetu ya vijana chini ya umri wa miaka 17,”.

Habari kwa hisani ya Bin Zubeiry

Tuesday 1 November 2016

AZAM YOUTH ACADEMY KUSAKA VIPAJI ZANZIBAR WIKI HII


VIJANA 12 kutoka mikoa ya Morogoro na Dodoma wamechaguliwa kwenye mchujo wa kusaka wanasoka chipukizi wa umri chini ya miaka 17 (U-17) ulioratibiwa na klabu ya Azam FC Uwanja wa Jamhuri, Morogoro jana.

Zoezi hilo linalosimamiwa na Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana Azam FC, Muingereza Tom Legg, lilihusisha vijana 528 huku 32 kati ya hao wakiingia fainali kabla ya kuchujwa na kupatikana waliobora zaidi 12.

Vijana hao 12 wanafanya idadi kamili ya vipaji vilivyochaguliwa kwenye mchujo wa awali kufikia 37 kati ya vipaji 2,073 vilivyofanyiwa usaili, wengine wakipatikana mikoa miwili ya awali ya Dar es Salaam na Tanga.

Wikiendi hii zoezi hilo la kusaka vipaji litaendelea tena kwa kufanyika Kisiwani Unguja, Zanzibar ndani ya Uwanja wa Amaan, Jumamosi ijayo Novemba 5 kuanzia saa 1.00 asubuhi hadi saa 9.00 Alasiri.

Kwa vijana waliozaliwa kati ya mwaka 2000, 2001 au 2002 waishio Zanzibar katika Visiwa vya Unguja na Pemba, wanaombwa kufika kwenye majaribio hayo ya sita kufanyika.

"Tafadhali unaombwa kufika na nakala ya cheti chako cha kuzaliwa kwa wale wote watakaokuja kwenye majaribio hayo,"imesema taarifa ya Azam na kuongeza; "Kwa majaribio mengine ya wazi kuhusu sehemu, tarehe na muda, tutawatangazia hivi karibuni,".

Thursday 20 October 2016

MSIMAMO WA LIGI KUU YA ZANZIBAR KANDA YA UNGUJA

Msimamo ulivyo katika ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Ungoja

 Orodha ya wafungaji wanaoongoza katika ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja

Tuesday 18 October 2016

ECOLE DE FOOT WANA SIMBA MAMOUDZOU WAGENI WA O.F.A ZANZIBAR

Kituo cha kukuza soka kwa vijana nchini kimewapokea wageni wake vijana wenye vipaji vya hali ya juu ECOLE DE FOOT WANA SIMBA MAMOUDZOU   U/12   -  U/14  kutoka nchini COMORO  katika kuanzisha uhusiano na ushirikiano kati ya pande mbili hizo.

Vijana hao wadogo wenye vipaji ambao ni tegemeo la baadae katika soka barani Africa wameanza mazoezi rasmi na wanatarajiwa kucheza michezo kadhaa ya kirafiki nchini Zanzibar pamoja na kupata nafasi ya kutembelea sehemu kadhaa za visiwa hivyo.

Tunaomba Wanzanzibar na watanzania wote kwa ujula kutoa ushirikiano wao kwa ndugu zetu hawa ambao wameonyesha hisia zao zote za kutaka kuwaendeleza vijana hawa ambao ndio mafanikio ya bara letu hili kwa siku zijazo.
Tunatoa shukurani kwa wale wote wanaofuatilia kwa karibu ujio wa vijana ECOME DE FOOT WANA SIMBA MAMOUDZOU  tokea kufika kwao, mazoezini, pamoja na mechi hadi pale watakapokamilisha ziara hii ya Kimataifa .

Kwa niaba ya Orange Football Academy inakaribisha msaada wa aina yoyote kwa wageni wetu ambapo mtoaji anaweza kuwaona wageni hao moja kwa moja na kutoa msaada wowote ambao mtoaji ataona kuwa utawasaidia vijana hao wadogo ambao ni wageni wa taifa zima kwa ujumla.

Tunatoa shukurani za dhati kwa wale wote wanaoendelea kutoa ushirikiano wao wa chipukizi hawa kwa wakati wote watakapokuwa hapa nchini.